Microsoft wametambulisha rasmi Windows 8 Jumanne mbele ya maelfu ya software developers waliokuwa wamekusanyika kwenye makao makuu ya jengo la kampuni hiyo Build, huko Anaheim, Califonia. Microsoft wamesema "wanailetea dunia kitu kitakachobadlilisha jinsi tunavyotumia PC." Windows 8 ina interface mpya kabisa, itakayofanya kazi kama touchscreens kwenye mobile devices kama tablets.
Kwa ujumla utakuwa na komputa ya kisasa inayojumuisha uzuri wa tablets wakati ukiwa bado unafurahia ufanyaji wa kazi wa komputa uliouzoea kama kawaida.
Windows 8 imetengenezwa kuwa "touch first, lakini itaendelea kutumia mouse and keyboard," alisema Steven Sinofsky, raisi wa Microsoft's Windows division.
Kwenye video hapa chini Boss wa kamouni Microsoft Steve Balmer anazungumzia mategemeo ya wapi Microsoft itakuwa miaka 10 ijayo.
0 comments:
Post a Comment