Friday 26 August 2011

Ni rahisi mtu mwingine kuingilia simu yako. Phone Hacking Lesson!


Wiki kadhaa zilizopita tuliona jinsi ambavyo Rupert Mudoch na kampuni yake ya News of the World ilivyoingia matatani kutokana na wafanyakazi wa kamouni hiyo kuingilia na kusikiliza voicemail za watu bila idhini ya mwenye simu. Siko hapa kuizungumzia kesi hii ambayo bado inaendelea. Leo nataka tuelimishane kwa kujibu maswali matatu kama ifuatavyo: phone hacking ni nini au inamaanisha nini?; Je, ni vipi mtu anaweza kuingilia simu yako na kufanya anachokitaka?; na mwisho utajikinga vipi katika kujiepusha au kupunguza wewe mwenyewe usiwe victim wa phone hacking? Naomba niweke wazi kwamba nia yangu si kuwaelimisha wahalifu jinsi ya kuingilia simu za wengine bali ni kuielimisha jamii jinsi unavyoweza kujikinga.

Phone hacking ni nini?

Hiki ni kitendo cha mtu kuingilia na kuchukua siri zilizoko kwenye simu yako bila idhini yako. Kwa mfano mtu anaweza kusikiliza voicemail ulizoachiwa na marafiki zako kwa kutumia simu nyingine bila wewe kujua. Katika mkondo wa sheria hili ni kosa na mtuhumiwa anayepatikana na hatia ataadhibiwa. Vile vile hii si nzuri (it is morally and ethically wrong). Imagine kama kila mtu angeingilia kwa siri na kusoma email, messages na hata kusikiliza voicemail za wengine, haki za mtu zitakuwa wapi? Anyway nia yangu si kuzungumzia mambo ya ethics na human rights, hii nawaachia wataalamu wa mambo hayo kujadili.

Ni vipi phone hacking inafanyika?

Kutokana na nafasi nitazungumzia phone hacking ya voicemail. Kuna njia mbili kuu.

Njia #1 – PIN namba za dharura (defaults PINs)

Kila voicemail ina PIN namba, infact kila unapotaka kusikiliza voicemail yako ulitakiwa kuingiza PIN. Hata hivyo kuondoa usumbufu kwa wateja haufanyi hivyo kwa sababu mitambo ya simu hugundua moja kwa moja kwamba hiyo ni voicemail yako kwa kuangalia namba uliyotumia kupigia. Ndio maana huwezi kusikiliza voicemail ya X kwa kutumia simu ya Z. Lakini itakuwaje kama simu ya X ina matatizo wakati ana voicemail muhimu ya kusikiliza? Au itakuwaje ikishukiwa kwamba X ni terrorist na wazee wa ulinzi wanataka kujua nini kimesemwa kwenye voicemail zake? Kutokana na hali hii makampuni ya simu yana publish online PIN namba ya dharura ili mteja aweze kuaccess voicemail zake kama kuna tatizo (remote access).

Ili kuweza kusikiliza voicemail katika hali hii makampuni ya simu yametoa namba unayotakiwa kupiga. Kwahiyo X anaweza kutumia simu ya Z kupiga kisha atatakiwa kuingiza default PIN…hureeee unasikiliza voicemail yako. Kwa bahati mbaya mtu mwingine mwenye nia mbaya anaweza kutumia njia hii na kusikiliza voicemail zako.

Njia #2 – Kupiga simu iliyoko engaged

Kama unayempigia simu hapatikani na unatakiwa kumwachia voicemail, ni rahisi kutumia njia hii kusikiliza voicemail yake kama unaijua PIN yake au kama hana PIN basi unatumia default PIN ya kampuni  ya simu anayotumia

Majaribio (watu watatu X, Y, Z)

X ampigie Y. Wakati X na Y wakiwa kwenye mazungumzo, Z ampigie Y. Z atapata ujumbe unaomtaka aache voicemail kwa sababu Y yuko kwenye simu nyingine. Z abonyeze * (star) kwenye simu yake. Hii itamuuliza PIN namba. Kwa kutumia default PIN anu PIN ya Y, Z ana uwezo wa kusikiliza voicemail za Y moja kwa moja.

Utajikingaje?

Ukitaka usiingiliwe hakikisha unaset up PIN kwenye voicemail yako. Tatizo ni kwamba utatakiwa kuiingiza kila mara unapotaka kusikilia voicemail. Kwa bahati mbaya siku hizi kuna software tools zinazoweza tumiwa na wahalifu wakai reset PIN yako bak to default. Hata hivyo hackers kila siku wanakuja na mbinu mpya hivyo tuzidi kuelimishana.

N.B. Kampuni nyingi za simu Tanzania hazitoi voicemail service. On one side hii ni nzuri kwa uasalama wa wateja wao.

Una maoni uma ushauri gani utakaoielimisha jamii kuhusu swala hili? Changia.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

 
Design by Goodluck Mboya | Bloggerized by IT4Dev - Premium Design