Thursday 25 August 2011

Google waja na yao, Je? Huu ndio mwisho wa facebook.

Facebook Vs Google+.



Google wako mbioni kuzindua social networking website itakayojulikana kwa jina la Google + (google plus). Habari hizi zimezua mzozo kwa wapenzi wengi wa social networking. Kwa die hard fans wa facebook bado wanaamini kwamba Google watachemsha na facebook itaendelea kushamiri. Wengine wanaona kama huu ndio mwanzo wa facebook kupoteza umaarufu ilionao duniani kote. Hapa nitajaribu kuchambua swala hili na kufafanua kwa wapenzi wa teknolojia kwamba wategemee nini.

Kwanza kabisa Google wametoa toleo la majaribio (beta version) na wanaoweza kuitumia kwa sasa ni wale wenye mwaliko rasmi kutoka Google. Hii nadhani ni mbinu ya kwanza ikiwa na nia ya kuwatamanisha wapenda kuchati kujua nini kilichomo kwenye platform hii. Nakiri kwamba baada ya kuiona na kuijaribu, Google+ is really cool.
Hata hivyo ni vigumu sana kujua kama Google+ itaitikisa Facebook au la. Ikumbukwe kwamba Google kwa muda mrefu wamekuwa na social networking ijulikanayo kama Orkut, ambayo haijaweza kupata umaarufu wowote isipokuwa kwenye nchi kadhaa kama India n.k. Kwa maoni yangu jina Orkut lenyewe is awful. Anyway tuisahau Orkut kwa maana sidhani kama hata Google wenyewe wanikumbuka.
Facebook wamejizatiti sana kwenye soko la social networking. Ni wabunifu wamekuwa wakiibadilisha plartform yao mara kwa mara ili iendane na mahitaji ya wapenzi wake. Japokuwa Google bado ni bingwa wa Internet overall, kushamiri kwa Facebook kumepunguza mapato kwa kiasi kikubwa. Google hupata mapato yake kwa njia ya matangazo (Google Ads) lakini tangu Facebook na wao kuanzisha Facobook Ads watoa matangazo wana choice. Hii ndio sababu kubwa Google wameamua kupambana na Facebook.
Hakuna anayepinga kwamba kuna anayeweza kushindana na Google search engine kwa sasa. Hata hivyo kitendo cha Google kutaka kuingilia market iliyotawaliwa na Facebook inawezaleta matatizo. Wengi wanaweza kuamini kwamba Google wanaikopi (clone) Facebook hivyo kuna haja gani kuiacha Facebook na kujiunga na kopi yake? Lakini wengine wanaamini Google wanaweza kukopi na kulea mapinduzi kwenye soko hilo. Ni vigumu kujua nini kitatokea ila maelezo hapo chini yanaweza yakakupa picha.

Mazuri ya Google+
  1.  Google+ imedhamiria kuongeza privacy measures wakati Facebook wamekuwa wakisuasua katika hili (kwa mfano kwenye facebook ukituma comment kila aliye kwenye profile yako anaona)
2.      Google+ ni kama combination ya facebook na twitter katika platform moja

3.      Google+ ni rahisi na nzuri kutumia  - labda kwa sababu bado mpya

4.      Google+ chat ni nzuri na engaging.

5.      Google+ ina ‘hangout’ ambayo ni video application – facebook wameweka yao muda si mrefu
Mabaya ya Google+
1.      Kusema kweli Google+ haina jipya zaidi kwa mtu wa kawaida ambaye hajali mambo ya privacy

2.      Google+ haina jina tunapoongelea social networking. Inajulikana kama product ya Google sio kama tunavyoiona facebook kama pure social networking site.

3.      Kuna features nyingi ambazo Google haina
Una mawazo gani kuhusu vita hii ya social networking? Toa maoni yako.

4 comments:

Anonymous said...

Mawazo yangu ni kwamba vita hii ni nzuri kwetu watumiaji. Pale mmoja anapoona mwenzake anafanya kitu isivyo mwingine anasaize opportuniy kuboresha, sisi wateja tunafaidika.

Anonymous said...

Alex Chizzar!
oooh...afadhali google mmeingia huku, maana ninaiamini sana kwenye masuala ya privacy..hata mails zao nazipenda, ninatumaini watafanya vizuri, though wanayokazi sana kuingia kwenye soko ambalo tayari facebook wameliteka, wanahitaji kuwa wabunifu na kuitangaza sana...itasaidia mtu kuwa na option nzuri zaidi ya social networking badala ya dominance ya fb...VIVA gOoGle

Anonymous said...

Nakubaliana na Alex, tunawahitaji google ile kuwatikisa facebook kama wao walivyowafanyia MySpace. Pia naamini google wana uwezo, mbinu na njia ya kushindana na facebook ipasavyo. C'mon GOOGLE.

Anonymous said...

...nadhani atakae kuja na control nzuri hasa privacy na uwezo wa kudhibiti kuhack accounts za watu basi atashinda hii vita..
kifo cha facebook hakitakuwa rahisi kama cha hi5

ila naona kama Google watapambana na wengi akiwemo twitter


jahaclassic

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

 
Design by Goodluck Mboya | Bloggerized by IT4Dev - Premium Design