Thursday 25 August 2011

Kuna faida yoyote(Added Value) kutumia facebook kwenye kampuni yako


Nimekuwa nasikia maelezo kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa kwamba matumizi ya facebook kwenye kampuni zao yamesaidia mahusiano yaliyopo kati ya kampuni na wateja wao, hawaoni kama kuna faida yoyote kutumia facebook baina ya wafanyakazi (internally). Wanasema kwamba wafanyakazi wanapoteza muda mwingi kuchati mambo yasiyo na uhusiano na kazi hivyo kuipotezea kampuni mapato. Hata hivyo nadhani wafanyabiashara hawa wanasahau faida ya mawasiliano inayoletwa na facebook. Research zinaonyesha kwamba mawasiliano ya jamii ni muhimu katika kuinua vipaji na kuleata maendeleo ya ujuzi wa mtu. Ndio maana tunaona makampuni mbalimbali yakitumia facebook nje na ndani ya kampuni.

Kwanini mawasiliano kazini?
Tsai na wenzake wamechapisha majibu ya ufumbuzi waliopata  kwenye study waliyofanya unaoeleza faida ya mawasiliano ya jamii (social interaction). Katika moja ya chapisho, wamegundua kwamba uboreshaji wa mawasiliano baina ya wafanyakazi umesaidia kuongeza ufanisi. Vilevile imeonyesha kwamba kwa kuruhusu vitengo mbalimbali katika kampuni kubadilishana mawazo kunapelekea ushindani kuongezeka ndani ya kampuni hivyo kusababisha ongezeko la uzalishaji.

Uchunguzi mwingine uliofanywa na Gallup umezidi kuonyesha umuhimu wa mawasiliano kazini. Katika majibu waliyopata kutoka kwa wafanyakazi mbalimbali kwa njia ya questionnaires, imeonyesha kwamba wafanyakazi wenye marafiki kazini wanajishughulisha na kujitolea zaidi ya wale wasio na marafiki zao kazini. Kama wafanyakazi wanajishughulisha kwa bidii ni dhahiri kwamba uzalishaji utaongezeka. Vile vile hali hii inasaidia kupunguza wafanyakazi kuhama mara kwa mara (staff turnover).

IBM wamekuwa wakitumia Beehive ambayo inafanana na facebook ili kuboresha ukaribu baina ya wafanyakazi. Kama ilivyo facebook, Beehive inatengeneza profile ya kila anayejiunga. Katika page, mwanachama anaweza kuorodhesha status yake kuonyesha wapi alipo na nini anchokifanya hivyo wengine wanajua jinsi ya kumpata. Pia wanachama wanaweza kupost picha, kupeana habari na hata kupanga na kutangaza events mabalimbali. Beehive imeonyesha kuboresha mahusiano baina ya wafanyakazi na kuleta ukaribu katika kutatua matatizo mbalimbali.

Kwa ufupi
Matumizi ya social networking ndani ya kampuni yanasaidia kuongeza ukaribu baina ya wafanyakazi. Social networking inaleta mabadiliko ya kiutamaduni na urafiki kwenye kampuni. Inawawezesha wafanyakazi kugundua wale wenye interest kama zao hivyo kuleta urahisi kubadilishana mawazo na kuelimishana.

Je? Wewe una mawazo au uzoefu gani wa swala hili. Changia hapa

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

 
Design by Goodluck Mboya | Bloggerized by IT4Dev - Premium Design