Tuesday 23 August 2011

Kitu kipya Verzo mitamboni

Je, uko tayari kujua kidodo kuhusu simu ambayo hujawahi kuiona au kuisikia? Najua uko tayari. Kampuni mpya ya simu ya Verzo imepania kutoa kitu chake kipya kitakacholeta ushindani mkubwa kwenye soko la simu. Verzo wamekuwa wagumu kutoa maelezo kuhusu simu hii mpya hata hivyo kama kawaida, exclusive on our blog, tumebahatika kupata picha za simu hiyo inayotegemewa kuzinduliwa mwezi wa tisa mwishoni.


Verzo wanaanza kufyatua simu zitakazoitwa Kinzo zinazotumia software ya Android.  Kwa maelezo tuliyopata simu hii mpya inatengenezwa na kampuni ya Novague. Inasemekana User Interface yake itakuwa ya kipekee. Nia na madhumuni ya kubadilisha UI ya simu hii kwa mujibu wa mtu wa ndani sio kujitenga na wengine bali ni kwa nia moja tu "kuhakikisha kwamba inafanya kazi viruri sambamba na system ya Android ilivyotengenezwa."
Wamiliki wa kampuni ya Verzo wanakataa katukatu kujaribu kusema kwamba wao kizazi kipya cha Samsung au Apple bali wankiri kwamba simu yao itakuwa nyembamba zaidi, inayofanya kazi kwa ufanisi, na kwa ufupi...bora zaidi kwa sasa.
Verzo wamepanga kuhakikisha kwamba wana chukua maoni kutoka kwa watumiaji wa simu ili kujua ni nini wanachopendelea na nini wasichopendelea. Wanategemea kuuza simu zao kwanza kupitia website yao kabla hawajaanza kuzisafirisha simu zao kwenda US na Europ na baadaye Russia, South America na Middle East mwishoni mwa 2011 au mwanzoni 2012.
Mwisho wa haya mapambano ya simu ni lini? Je, Africa inayosemekana ina soko kubwa la simu mbona haijatajwa hapo juu? Changia hoja na toa maoni yako sasa.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

 
Design by Goodluck Mboya | Bloggerized by IT4Dev - Premium Design