Tuesday 23 August 2011

Apple kuzindua toleo rahisi la iPhone 4 wiki nne zijazo


Wakati ambapo wapenzi wa vitu vikali vya kisasa duniani wakiwa wanasubiri kwa hamu ujio wa toleo jipya la iPhone 5 kutoka kwa Apple, Reuters wanaripoti kwamba Cupertino (mji maarufu wa wasomi Carlfonia na makao makuu ya Apple), wako katika hekaheka za kuboresha toleo lililopo sasa iPhone 4. Ikumbukwe kwamba Apple walitoa matoleo mawili tu ya iPhone 4 yaani 16G na 32G. Sasa wazee hawa wa kazi wamedhamiria kuleta toleo litakalokuwa rahisi zaidi lenye storage space ya 8G. Kwa mujibu wa wasaka habari za chinichini kampuni moja ya Korea imelamba cotract hii na wakati tukiwa tunakwenda mitamboni kazi za kufyatua parts kwa ajili ya toleo hili rahisi zinaendelea. Inategemewa toleo hili litakuwa madukani wiki kadhaa zijazo.
Kwa wapenzi mnaosubiri iPhone 5 series, msaka habari ameelezwa kutoka kwa mtu wa ndani wa Apple kwamba toleo hilo jipya linalotegemewa kuzinduliwa mwishoni mwa mwezi wa tisa litakuwa na touchscreen nzuri zaidi, antenna yenye nguvu zaidi na kamera ya 8M. Kampuni ya Hon Hai and Pegatron zimepewa taarifa kujiweka tayari kulipua simu 45 million na kuzisamabaza duniani kote. Kama kawaida habari kama hizi huwa finyu na zisizojitosheleza hata hivyo tutazidi kuwarushia maelezo kadri tunavyokuwa tunazipata nyepesi nyepesi.

2 comments:

Anonymous said...

Kama iPhone 5 karibia itoke kuna haja gani ya kununua iPhone 4. Ok labda bei itakuwa rahisi lakini tukumbuke Apple wana ushindani mkubwa sana sasa hivyo sidhani kama iPhone 5 itakuwa ghali hata kidogo

emu-three said...

Mhh, mamno ya kisasa hayo.Tupo pamoja wakuu

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

 
Design by Goodluck Mboya | Bloggerized by IT4Dev - Premium Design