Sunday 28 August 2011

Wapenzi wa techno (watekno), iPhone 5 inatoka. Tutegemee nini?

Tetesi kuhusu toleo jipya la iPone 5 next generation limekuwa likizidi kwa wiki kadhaa sasa. Ninafuatilia kwa karibu nyendo za toleo hili na ninaweza kusema wataalam wa Cupertino - Apple wanakaribia kutoa toleo hilo jipya kama siyo mwishoni mwa mwezi wa tisa basi itakuwa mwezi wa kumi.

Ni juzi tu DigTimes wametoa report kwamba Pegatron (wafyatuaji wa iPhone 5) wanaanza kuzisafirisha simu million 10 kwenda kwa wasambazaji wakuu. Repoti ya awali kutoka DigiTimes ilisema kwamba Pegatron wamepokea oda ya units million 15 lakini sasa inasemekana ni units million 10. Pia kupunguzwa kwa bei ya iPhone 4 kunaashiria kwamba iPhone toleo jipya litatoka hivi karibuni hivyo watekno kaeni mkao wa kula.


Apple wamekuwa wakiweka bidii kubwa sana mwaka huu kuboresha software zinazotumika kwenye product ambazo ni iOS (kwa ajili ya mobile devices) na Mac OS (kwa ajili ya PC za MAC). Kwa sababu hiyo, tutegemee iPhone 5 inayo respond haraka, inayocheza video na kuonyesha picha vizuri zaidi. Hii itahusisha 1080 HD (picha za quality ya juu) na kamera iliyoimarishwa. Imesemekana pia kwamba kampuni inayotengeneza makasha (covers) za iPhone imeshapokea michoro ya kasha jipya, kuna tetesi  kwamba tunarudi kwenye iPhone za kizamani. Hii inamaanisha kasha la iPhone 5 linawezakuwa curved kama la iPhone 3G. Hata hivyo itakuwa na screen ndogo zaidi 4-inch.
Video hapo chini inaonyesha features ambazo wengi wanaamini kitu hicho kipya kitatuletea.

Habari hii inakuja siku kadhaa baada ya aliyekuwa CEO wa Apple bwana Steve Jobs kuachia ngazi pamoja na habari kwamba matoleo mapya ya iPad 3 na iMac yako karibu kufyatuliwa.

0 comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

 
Design by Goodluck Mboya | Bloggerized by IT4Dev - Premium Design