Virus kwa ufupi
Ni program kama program nyingine za komputa. Tunaposema program ya komputa inamaanisha kwamba mtaalamu wa kuandika program ametumia ujuzi wake kuandika program inayoweza kutumika kwenye komputa kama vile Microsoft Word n.k. Hata hivyo hii si program ya kawaida. Nia na madhumuni yake huwa si mazuri na madhara yake yanaweza kuwa makubwa. Kwa mfano komputa yangu ilipoingiliwa na virusi wakati nafanya project ya mwisho ya degree, nilipoteza kazi yangu siku mbili kabla ya kukabidhi baada ya virus kuingilia komputa yangu. Kwa bahati nilikuwa nimeweka back up kwenye flash memory. Hata hivyo back up haikuwa up-to-date hivyo ilinichukua masaa zaidi ya ishirini na tano kuongeza yale niliyopoteza. Masaa haya yangeweza kutumika kwenye kuiboresha project sio kufanya upya vitu ambavyo nilishavifanya.
Kwa kifupi virus ni kipande kidogo cha software program kinachojishikilia kwa siri kwenye program za kweli tunazotumia kila siku. Kwa mfano kama unatumia Microsoft Excel (Spreadsheet) hako kamdudu kanaweza kuwa kamejibanza kwenye hii program. Kila unapoifungua Spreadsheet unajikuta umefungua hicho kiprogram bila kujua.
Kwa kifupi virus ni kipande kidogo cha software program kinachojishikilia kwa siri kwenye program za kweli tunazotumia kila siku. Kwa mfano kama unatumia Microsoft Excel (Spreadsheet) hako kamdudu kanaweza kuwa kamejibanza kwenye hii program. Kila unapoifungua Spreadsheet unajikuta umefungua hicho kiprogram bila kujua.
Virusi vya komputa vinafanya kazi vipi?
Email Viruses- Watu wengi hivi karibuni wamekuwa wakipata virusi vya kwenye email (e-mail viruses). Email virus anajificha kwenye email na kusafiri nayo kama attachment kwenye message. Virus huyu ana uwezo wa kujiongeza (raplicates itself) hivyo anaweza kujituma mwenyewe kwa kutumia email yako kwenda kwa watu wote walio kwenye contact zako. Hata hivyo virus huyu hawezi kufanya kazi mpaka ufungue attachment au link iliyoificha. Hivyo kama umepokea email yenye virus, bado hawezi kufanya chochote mpaka utakapofungua attachment au link iliyomficha. Kwa sababu hiyo kuanzia leo USIFUNGUE email attachment au links kama huna uhakika. Mtumie email rafiki aliyekutumia uhakikishe kama ni yeye aliyetuma.
Trojan Horses – Hawa ni pia ni komputa program. Program inajifanya kuwa program ya kawaida ila unapoifungua tu inaingia na kujificha kwenye hard disk ya komputa yako. Ana tabia ya kufuta kila kitu kilichopo kwenye hard disk na hata kuharibu operating system hivyo kuiua komputa yako kabisa. Tofauti nyingine kati ya email virus na huyu Trojan ni kwamba Trojan hawezi kujiongeza (can not replicate itself).
Worms – Hawa wana tabia ya kutumia komputa network kujiongeza na kutafuta komputa ya mtu siyo na vikingaji (antvirus program) ili waingie.
Kwa nini watu wanateneza virus?
Unaweza kujiuliza ni kwa nini watu wanatengeneza virus! Ukweli ni kwamba kuna sababu kama mbili:- Uharibifu - Kuna watu wanpenda kuharibu na kuona wengine wanahangaika kutafuta solution kwa kitu ambacho amekifanya yeye
- Sifa ya kuvumbua - Kila mtu anapenda kuwa kama Isaac Newton. Kuacha historia kwamba waliweza kuitingisha dunia na kufanya kitu ambacho weni hawajakifanya.
Kuna njia kadhaa:
1. Kama una hofu kubwa sana ya virus basi tumia operating system yenye kinga zaidi kama UNIX. Ni vigumu sana kusikia virus wameingilia operating system ya UNIX kwa sababu ya kinga mbali mbali zilizotengenezewa ndani.
2. Kama unatumia operating system nyingine yeyote basi hakikisha unaweka vikinga (ant-virus - virus protection software). Unaweza kupata kopi ya bure hapa.
3. Usiamini program nyingi unazozipata kwenye internet, nyingi zina virus isipokuwa program unazopata kutoka kwa watengenezaji wenyewe wanofahamika. Wakati mwingine nunua program iliyo kwenye CD kuliko kuchukua (download) moja kwa moja.
4. Usifungue email attachment bila kuwa na uhakika.
5. Hakikisha umeruhusu (enable) Macro Virus Protection (angalia maelezo hapo chini) kwa wanaotumia Microsoft applications. Pia usiruhusu macros unapofungua document. Macro hazihitajiki kwenye document hivyo ukipokea document yenye macro jiulize ni kwa nini kabla hujaruhusu.
Jinsi ya kujikinga na Macros unapotumia Microsoft Word (maelezo haya ni kwa version mpya za Microsoft Office)
i. Go to ‘File’
ii. Click Options
iii. Click Trust Center
iv. Click Trust Center settings
v. Click Macros
vi. Set the settings as shown
Kama una swali ama unataka maelezo zaidi wasiliana nasi kwa kandika comment hapa chini
Kila la kheri
8 comments:
Kwann ao waddu wako wka wins na sio linux au unix au mac? Kwan vrs anapo tengnzwa wanjua mifumo gan ya pc au mac htkp anapo tengnzwa wanjua mifumo gan ya pc au mac htkp
Linux inasadikika kuwa ndiyo Operating System yenye uwezo mkubwa wa kuzuia virus na security attacks nyingine. Sababu kubwa ni kwamba Linux haitengenezwi na wafanyakazi wachache wa kampuni fulani kama zilivyo Windows na nyinginezo. Linux ni open source ikimaanisha kwamba mtu yeyote ana uwezo wa kuona (code) jinsi ilivyoandikwa. Hata wewe kama una utaalamu una uwezo wa kuipitia software hiyo na pale unapoona pana tatizo unatoa solution au maoni yako. Maoni hayo yanapitiwa kama kawaida na watu mamilioni duniani kote na kuchangia au kukosoa. Sasa mwisho wa siku kutokana na mawazo, ujuzi na utaalamu uliowajumuisha watu zaidi ya million toka duniani kote, inapatikana software iliyo imara na inayoweza kujikinga vizuri zaidi. Hii ndiyo maana Linux ni nzuri.
Hata hivyo kuna wengine wanaamini kwamba Windows inasumbuliwa sana kwasababu kuna watu wanoichukia hivyo wanataka kuiharibia jina.
Utaamua uamini kipi lakini ukweli ni kwamba hadi sasa Linux haijsumbuliwa sana na matatizo ya virus kama ambavyo Operating Systems nyingine zimekuwa zikisumbulliwa.
Natumaini umepata jibu linaloridhisha
Ndio Mzee.,Pamoja na hilo o.s nyng unauwezo wa kuinstall sftwar/prgm/games lakin LINUX mf. UBUNTU10 unapatiwa package nzm kam updater.,kila uingapo net. Huna uhuru wa add/rmv prgm.. Nami nataman tumia web brwser ingn kwa ubuntu mbali na mozilla..twar/prgm/games lakin LINUX mf. UBUNTU10 unapatiwa package nzm kam updater.,kila uingapo net. Huna uhuru wa add/rmv prgm.. Nami nataman tumia web brwser ingn kwa ubuntu mbali na mozilla..
Sasa hapo ndio matatizo au drawbacks za Linux zinapoanzia. Linux ni wazuri kwenye mambo ya security lakini bado hawajaweza kuifanya software hii kuwa useful kwa mahitaji mbalimbali kama zilivyo Operating Systems nyingine.
Hata hivyo napenda ukumbuke kwamba dunia inaelekea kwenye service kama wanazotoa Linux, kwamba huhitaji kuu-install software zote kwenye system yako, una uwezo wa kuzipata na kuzitumia pale unapohitaji tu kwa njia ya Internet. Hii inaitwa 'Cloud Computing' - Soma habari hii kamili leo kwenye blog yako hii ya teknoloji.
Hata hivyo Windows bado ni superior kwenye mamboa mengi kama vile interface.Grafical User Interface ni nzuri na robust. Kwa sababu hizi na nyingine ndio sababu Linux haitumiki sana kwa matumizi ya kawaida ukilinganisha na Windows
Kama unataka kujikinga na Macros kupitia Microsoft office ya 2007 unajikina vipi?
nawashukuru kwa elimu mnayotoa, mimi nimewahi kutumia ubuntu, lakini tatizo kubwa nililoliona ni operating system inayochagua sana software, kwanini wasingetengeneze iwe free kwa kuinstall program unazotaka kama ilivyo Window XP? Hii nadhani ni sababu inayofanya isitumike sana kwa huo ugumu uliopo,inasapoti software chache na nyingi inakataa, mfano illustrator yenye ua, quark 6 na nyinginezo za graphics.Naomba msaada kwa hilo. Musa Ngarango Mob:0715 283 001 E-mail:katunikwanza@gmail.com
Mambo yanabadlilika, hata Microsoft wanabadili jinsi OS zao zinavyofanya kazi. Kwa maswala ya graphics kama ni kwa ajili ya website CSS3 na HTML5 zitatumika zaidi. Musa Ngarango umejaribu GIMP? Nitakutumia email ila kwa faida ya wote link hii hapa: http://www.gimp.org/. GIMP ni free graphics application na rahisi kutumia. Inafanya kazi vizuri tu kwenye Ubuntu. Kama unataka Adobe suite tuwasiliane.
Post a Comment