Thursday, 25 August 2011

Windows 8 kutikisa soko la teknolojia


Kama unafikiri una toleo jipya la Operating System (OS) kwa sababu PC au laptop yako ina Windows 7 inabidi ujiulize tena. Microsoft wametoa tangazo kwenye kongamano la D9 kuhusu toleo jipya la OS linalojulikana kama Windows 8 next generation. Windows 8 inategemewa kuwa ya kipekee na tofauti kabisa na matoleo mengine. Hii ni mara ya kwanza OS kwa ajili ya desktop PC inatengenezwa kuwa nyepesi na rahisi kutumia kama zilivyo OS za simu za mkononi. Itakuwa touch-screen inayoweza kutumika kwenye tablets, desktops na laptops.

Japokuwa toleo la majaribio (beta version) tayari iko mtaani bado hatujaweza kupata uhakika ni lini full version itaanza kupatikana kwenye PC au kuuzwa madukani. Tunaamini Microsoft wanataka kuhakikisha wanaitengeneza software hii katika kiwango cha juu sana ili kuepusha matatizo kama ilivyokuwa kwa Windows Vista. Hata hivyo haitachukua muda sana, toleo hili linalosubiriwa kwa hamu litakuwa mtaani kwenye miezi ya mwanzo ya mwaka 2012.

Jionee mwenye kwenye hii video toka kwa Microsoft.
#Version 2

#Version 2


Video hii kutoka kwa Jensen Harris, director wa program na management wa Microsoft inavutia. Apps zimepangwa kama tiles, zikimwezesha mtumiaji kuzisukuma pande zote na kuchagua app anayoipendelea. Nadhani vijana wa kisasa watavutiwa sana na hii feature kwani wao hawajaziona enzi zetu tulipokuwa tunatumia Windows 95.

7 comments:

Anonymous said...

Kwa hali hii mbona tunashindwa kujua cha kununua. Tafadhali wataalam mtufafanulie tofauti zilizopo

mimimkulima said...

....safi,OS zingine nzito sana...ila watu wa Hardware nao waendani na kasi hiyo ya applications kwani ule uzito wa OS zingine kama vista na win7 unachangiwa na HW....Ila pia watu wa applications zingine lazima nao waupdates SW zao hasa drivers mfano..HP printers CD drivers zinazokuwepo kwenye printer hazirun/incompatible na win7n so inakubidi udownload updates kwenye site yao ..sasa hiyo ni tatizo cuz inaweza kukuta unahitaji printer kijijini na net huna...


I love technology

Jahaclassic

Anonymous said...

Big up kaka hapo juu (coxlee13) great comment. Watanzania tuna watu wenye mawazo yanayoweza leta changes Tanzania na duniani kote. Keep it up

Anonymous said...

ai cant see the video above here where z it or jst give ne a link to follow in order to acces it...

Chief Editor said...

Sorry to hear that you can't access our videos here. One possible reason might be that you have not installed Adobe Flash Player on your system. Try to install one from the link below:
http://get.adobe.com/flashplayer/

Otherwise watch the video at:
http://youtu.be/p92QfWOw88I

Let us know how you are getting on...

anonymous said...
This comment has been removed by the author.
Chief Editor said...

Kagimbo karibu tushirikiane. Ni vizuri tukilink pamoja. Kwa upande wangu kutakuwa na orodha ya blog mbalimbali na kwenye moja ya kona ya blog hii hivyo tutakuweka hapo

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

 
Design by Goodluck Mboya | Bloggerized by IT4Dev - Premium Design