Kwa kutambua umaarufu na umuhimu wa lugha ya Kiswahili duniani, Microsoft wametoa pack ya Kiswahili kwa ajili ya Widows 7 na Microsoft Office. Pack hii inapatikana online na zaidi ya yote ni BURE. Akizungumzia toleo hili boss wa Microsoft Afrika Mashariki na Kusini bwana Louis Otieno alisema
“zaidi ya watu million 150 wanaozungumza Kiswahili Afrika sasa wanaweza kuanza kutumia technolojia kwa lugha waipendayo na kuielewa zaidi. Hii ni mojawapo ya njia za kupanua wigo wa lugha duniani”.
Tazama video ya ufunguzi huo hapa chini.
Viongozi na wabia mbalimbali Afrika na duniani kote wameipokea habari hii kwa furaha kubwa. Mkurugenzi wa elimu nchini Kenya mama Lydia Nzomo amesema Windows 7 ya Kiswahili ni ushindi kwa watoto wa shule za msingi kwani itawasaidia kujua kutumia komputa haraka.
Microsoft wanasema toleo hili litahamasisha serikali za nchi husika kuongeza uwekezaji kwenye mambo ya IT, kupunguza ujinga na kuwavutia watu wengi zaidi kutumia komputa hasa kwenye nchi hizi ambazo utumiaji wa komputa bado ni mdogo.
Kazi ya kutengeneza toleo la Kiswahili lilifanywa na wataaluma wa lugha ya Kiswahili kutoka Afrika mashariki na kati kwa muda wa miaka miwili. Aliyeiongoza kazi hii ni mtafasiri wa lugha ya Kiswahili ndugu Mpasua Msonobari. Mpasua alisema kuna maneno zaidi ya 300,000 yliyotafasiriwa kwa Kiswahili kwenye toleo hilo jipya.
Download kwa kubonyeza hapa kupata toleo lako la Windows 7 toleo la Kiswahili
Microsoft wamekuwa wakishirikiana na nchi mbali mbali Afrika na duniani ili kuzitambua na kuzitafasiri lugha mbalimbali.
Habari hii ni nzuri lakini watanzania tujiulize, je, kuna mtanzania aliyeshiriki katika kazi hii? Tanzania inaongoza na kusifiwa kwa kukienzi na kukiendeleza Kiswahili, kama hatujihusishi kwenye project kubwa kama hizi si kazi bure. Mpasua aliyeongoza kazi hii ni mRwanda-mKenya watanzania tuko wapi? Changia mawazo yako.
5 comments:
Tunajivunia maendeleo haya lakini kama mwandishi anavyosema jamani watanzania tuko wapi!!!!!!!!!!!!!!???????
MI NADHANI NIKUTO WAJIBIKA VIPI MICROSOFT IJE TANZANIA IMTAFUTE MTU AJUAYE KISWAHHILI WAKATI KENYA KUNA WATU WANAJIFUNZA KISWAHILI HADI CHUO ANAKISOMA MPAKA AKIANZA KUONGEA UNAWEZA UKASEMA LUGHA GANI HII KENYA WAMETUTANGULIA SANA TANZANIA TUNATAKIWA KUFANYA JITIHADA
Kuna tatizo kubwa hapa. Sio kwamba hakuna watanzania wenye ujuzi au wasio na big picture. Tatizo ni kwamba watanzania tunaridhika na tunakuwa tunasita kujaribu mambo mengi. Hatujiuzi na kujinadi. Tuna uwezo mkubwa kinachotakiwa ni kusonga mbele. Tuanze kwa kuwa recognise watanzania wenzetu wanaofanyavitu vya maana. Kitu kidogo kama hawa wanachapisha kwenye blog hii wanahitaji pongezi. Ni elimu inayosambaa kwa wengi
Mdau Sweeden
Aisee..mi niko hoi na Kiswahili kilichotumika kwanza kina misamiati migumu ambayo maisha yangu yote sijawahi kuona misamiati hiyo..Microsoft wajitahidi kurebisha hicho Kiswahili maana kitatupa shida sana ijapokuwa sisi wote ni wa Tanzania..na Kiswahili ni Lugha yetu..
Kagimbo ni kweli kwamba kiswahili kilichotumika hapa kinatisha. Hili ni swala tunalotaka kuanza kulivalia njuga ili Microsoft wajue na kutafuta njia za kurekebisha. Tutatoa habari hivi karibuni ya nini tunachoweza kufanya ili hili lifanyiwe kazi. Tunahitaji kuact haraka kabla Windows 8 haijatoka. Ushirikiano wetu utatusaidia.
Asante
Post a Comment