Monday, 29 August 2011

Kati ya Plasma, LCD, na LED TV : ipi bora zaidi?


Ikiwa karibia zisahaulike zile TV za kizamani (CRT) zilizokuwa kubwa nzito na zenye madhara, HDTVs zimekuwa ndio mtindo wa kisasa. HDTV ziko za aina tatu: Plasma, LCD na LED. Kutokana na hali hii watu wengi tunajikuta na maswali mengi pale tunapotakiwa kuchagua ni HDTV gani kununua kupendezesha nyumba zetu. Japokuwa kwa muda mrefu malumbano ya ipi ni bora zadi hayajapata jibu sahihi, Plasma TV ilipotoka ilikuwa inasifiwa kwa kuonyesha picha nzuri na inayong’aa.  
Hata hivyo LCD zilipoingia kwenye soko zilionekana ni nyembamba zaidi na za bei nafuu kutokana na teknolojia yake ya CCL backlight. Tofauti ya hizi aina mbili imekuwa ikihusu bei, ukubwa, uzuri wa picha na wembamba.

Miaka michache iliyopita kutokana na maendeleo ya kiteknolojia mshindi amepatikana yaani LED. LED inatumia umeme mdogo zaidi, na huwezi kupata TV nyembamba zaidi kama LED lakini kwa bahati mbaya ndio ghali kuliko zote. Kama una uwezo lipa zaidi na unapata HDTV bora kuliko zote ambayo inatumia teknolojia ya LED.

Tofauti kati ya LCD na Plasma

Plasma
 
1.       Plasma ni mshindi kwenye contrast ratio yaani kiasi cha mwanga (darkest dark and whitest white). LCD screen zimejitahidi sana kuboresha contrast ratio lakini bado teknolojia yake haijaweza kufikia ile ya Plasma
2.       Kwa video na moving  images basi mshindi ni Plasma. Japokuwa LCD inajitahidi bado Plasma inaongoza kwenye issue ya lag time au delay time. Kama lag time ya TV yako ni nzuri movie inaonekana smooth kabisa. Pia unaweza kuangalia picha kwenye Plasma kutoka kila kona. Hivyo kama huna nafasi yakutosha na baadhi ya viti vitakuwa upande wa kushoto ama kulia basi usinunue LCD maana utakuwa disappointed.

3.       Japokuwa imekuwa inkionekana kwamba TV kubwa zinakuwa na picha iliyofifia zaidi, Plasma kwa mfano ya inch 50 ni nzuri zaidi kuliko LCD

LCD

1.       Kama unataka kutumia TV yako kutazama picha za kawaida (still picture) kama ulizopiga wakati wa graduation yako basi LCD ndio TV ya kununua. Screen ya komputa yako inatumia LCD technolojia kwasababu inafanya kazi vizuri zaidi kwa kutizama still images.

2.       Kama unajali bili ya umeme basi LCD ndio mwendo. Pllasma TV zina neon gas ndani. Neon gas hii inahitaji kiasi kikubwa cha umeme kuitoa mwanga. LCD inatumia karibu nusu ya umeme unaotumika kwenye Plasma
3.       LCD ni bei nafuu zaidi ukilinganisha na bei ya Plasma

LED
Kwa ubora zaidi wa picha, wembamba na ukubwa wa TV basi LED ndio mwendo wa kisasa. Kutokana na teknolojia ya LED kuna uwezekano miaka kadhaa ijayo kukawa na toleo la LED lenye wembamba wa credit card.
Ushauri
Kwa sababu bei ya LED inapungua, hakuna haja ya kununua tekonolojia hiyo sasa hivi. Kama hela sio shida nunua ila kwa nini ulipe premium wakati miezi kadhaa ijayo utapata TV hiyo kwa bei nafuu zaidi?
You get what you paid for. Chaguo kati ya Plasma na LCD linategemea mfuko wa mtu. Kama utalipa zaidi utapata TV nzuri kuliko Yule aliyelipa kidogo. Hata hivyo kabla ya kununua TV yoyote, kama unajua model  nenda online usome feedbacks za watu.
Changia mawazo na ujuzi wako

3 comments:

Anonymous said...

Cool post, very useful

Anonymous said...

Thanks for the post everyday i find useful issue in this site.Thanks for the post everyday i find useful issue in this site.

Hosanna Inc said...

Its very Good Lesson especially for we Developing Countries

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

 
Design by Goodluck Mboya | Bloggerized by IT4Dev - Premium Design